Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho ametuhumiwa kulaghai na kukwepa kulipa kodi kati ya mwaka 2011 na mwaka 2012 wakati akiiongoza klabu ya Real Madrid.

Watoa mashtaka hao wamesema Mourinho alitenda makosa hayo akiwa katika klabu ya Real Madrid ambapo anatuhumiwa kukwepa kulipa kodi ya jumla ya €3.3m (£2.9m; $3.6m) katika miaka hiyo.

Maafisa hao pia wamewataja watu wengine wanaotuhumiwa kufanya ulaghai wakati wa kulipa kodi Uhispania kuwa ni Lionel Messi, aliyepatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miezi 21 jela.

Rais Mstaafu Olusegun Obasanjo wa Nigeria ampongeza Rais Dkt. Magufuli
Jaji Malecela wa Mahakama Kuu ya Tanzania aachia ngazi