Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kwenye ukumbi wa uwanja wa Do Dragão mjini Porto, walishangazwa na kauli ya meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ambayo iliendelea kudhihirisha kikosi cha The Blues ni bora kuliko FC Porto.

Mourinho aliutumia mkutano huo na waandishi wa habari kwa kutaka kuujuza umma wa soka duniani kwamba kikosi chake kilikua na ubora wa hali ya juu katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo, licha ya kukubali kisago cha mabao mawili kwa moja.

Mourinho alisema anashindwa kuamini kama kweli Chelsea wamepoteza mchezo dhidi ya Porto na hadhani kama ilikua sahihi kwao kupoteza mpambano huo ambao ulimrejesha nyumbani nchini Ureno tena kwenye klabu aliyoanzia kazi ya umeneja.

Alisema anaamini hakuna kilichoharibika kwake kutokana na kuamini kikosi chake kilicheza vyema na kudhihirisha ubora uliopo, lakini bahati ya ushindi haikua kwao baada ya kuelekea kwa wenyeji ambao walimaliza mchezo kwa furaha kubwa.

Ndikumana Amuhurumia Nyosso
Roma Adai Hajapata Barua Ya Wimbo Wake Kufungiwa, Awapa Ushauri BASATA