Aliyekua meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amewapongeza Leicester City kwa kufikia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini England.

Mourinho amesema hana budi kuungana na wadau wengine wa soka duniani kote kuwapongeza mabingwa hao wapya katika ligi ya England, kutokana na mazuri waliyoyafanya msimu huu.

Mourinho ambaye kwasasa bado hajapata kibarua tangu alipoondoka Stamford Bridge mwishoni mwa mwaka jana, ameongeza kwamba amefurahishwa na kazi ya Leicester inayoongozwa na meneja Claudio Ranieri.

Kwa mazungumzo ya Mourinho, anaonyesha kama angeendelea kubaki Chelsea na wachezaji wasingemsaliti, alikuwa na uhakika wa kuutetea tena ubingwa huo kwa mara nyingine.

Gundu Lingine Laibuka Msimbazi
Simba Yarejea Kisiwani Unguja Kupanga Mikakati Ya Jumapili