Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema itakuwa vigumu kucheza dhidi ya Manchester City wakiwa bila Sergio Aguero Jumamosi hii.

Mshambuliaji huyo wa Argentina, 28, amefungiwa kucheza mechi tatu baada ya kumpiga kiwiko cha mkono mchezaji wa West Ham,  mechi ambayo City walishinda 3-1.

Aguero amefunga mabao matatu katika mechi tatu alizocheza Ligi ya Premia msimu huu lakini Mourinho anasema kutokuwepo kwake kuna maana kwamba City, chini ya Pep Guardiola hawataweza kutabirika.

“Akiwa hachezi basi wana wachezaji wengine wengi wanaweza kucheza nafasi yake,lakini inakuwa vigumu zaidi kujua watajipangaje katika mechi ” amesema Mourinho.

Mourinho amesema mojawapo kati ya wachezaji wanaoweza kucheza nafasi hiyo ni pamoja na Kelechi Iheanacho, Raheem Sterling na David Silva anaweza kuchezeshwa na kocha Pep Gudiola kama nambari tisa kwenye debi hiyo Old Trafford

Mchungaji Rwakatale Atenga Milioni 25 Kwaajili Ya Kuwarejesha Wafungwa Uraiani
Mahakama Nchini Kenya Yaruhusu Wasichana Kuvaa Hijab Wawapo Shuleni