Mpambano wa nani mkali kati ya Jose Mourinho wa Manchester United, Pep Guardiola wa Manchester City na Antonio Conte wa Chelsea, umeanza kuchukua nafasi katika soka la nchini England, kufuatia mjina ya watatu hao kuwa miongoni mwa mameneja wanne wanaowania tuzo ya mwezi Agosti.

Mwingine aliopo katika orodha hiyo ni meneja wa klabu ya Hull City Mike Phelan ambaye ameonyesha kujitutumua vilivyo tangu kuanza kwa msimu wa 2016/17, ambapo kikosi chake kimefanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo miwili na kupoteza mmoja.

Jose Mourinho, Pep Guardiola na Antonio Conte wote kwa pamoja wameviongoza vikosi vyao kuibuka na ushindi katika michezo mitatu ya mwanzo, sababu ambayo imechangia kuingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya meneja bora wa mwezi Agosti.

Kabla ya kuanza kwa msimu wa 2016/17, wadadisi wa masuala la soka la nchini England walitabiri uwepo wa ushindani mkubwa miongoni mwa mameneja hao watatu ambao wamekabidhiwa vikosi vya klabu ambazo zimekua zikifanya vyema katika mshike mshike wa ligi kuu, na sasa imeanza kudhihiri.

Klabu za Chelsea, Man Utd pamoja na Man City zinashikilia nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa ligi ya England, lakini zinatofautishwa na mabao ya kufunga na kufungwa.

Picha: Waziri Mkuu azindua ripoti ya hali ya hewa barani Afrika
Jina La Bastian Schweinsteiger Lapitishwa Old Trafford