Aliyekua meneja wa klabu bingwa nchini England, Chelsea, Jose Mourinho hatakweenda likizo baada ya kuondoka Stamford Bridge.

Meneja huyo kutoka nchini Ureno, alifutwa kazi baada ya The Blues kufungwa michezo 9 kati ya 16 msimu huu.

“Hatokwenda likizo, hajachoka, hahitaji likizo,” taarifa kutoka kwa wakala anayemwakilisha Mourinho imesema.

“Anamatumaini sana na tayari anaganga yajayo.”

Mourinho alijiunga na Chelsea kwa mara ya pili Juni 2013 na msimu uliopita akawaongoza kushinda Ligi ya Premia na Kombe la Ligi.

“Jose Mourinho ana furaha kwamba alirejea Chelsea kwa sababu aliweza kuwapa mashabiki taji jingine la Ligi ya Premia, ligi ambayo hawakuwa wameshinda kwa miaka mingi,” taarifa ya Mourinho imesema.

“Anajivunia sana kushinda vikombe vinane akiwa Chelsea na anawashukuru mashabiki kwa muunga mkono vipindi hivyo viwili alikuwa katika klabu hiyo.

“Wakati wa maisha yake ya ukufunzi, Jose wakati mwingine amekuwa akiamua kuondoka katika klabu, lakini ni Chelsea pekee ambako klabu iliamua anafaa kuondoka.”

Pep Guardiola Ajisogeza Taratibu Etihad Stadium
Tanzania Yaendelea Kusubiri Miss World