Meneja wa Man Utd Jose Mourinho amelazimika kuwaomba radhi mashabiki wa Man Utd kufuatia shughuli kumuharibikia akiwa katika himaya ya waajiri wake wa zamani (Chelsea) kwa kukubali kufungwa mabao manne kwa sifuri.

Mourinho amefikia hatua ya kuwataka msamaha mashabiki wa mashetani wekundu kutokana na kuhisi huenda baadhi yao wakaaminii bado ana mapenzi na Chelsea, na kupoteza mchezo dhidi ya Man Utd hiyo jana hajakutilia maanani.

Mourinho amekiri kuumizwa na matokeo hayo kwa kusema hakuna asiyejua uchungu aliouhisi wakati mambo yalipowaharibikia katika uwanja wa Stamford Bridge, lakini ukweli utabaki moyoni mwake.

“Sina budi kuomba radhi kwa mashabiki wa Man Utd duniani kote, na niwahakikishie kwamba mimi ni Man Utd kwa asilimia 100, sio 99% wala 1% kwa Chelsea ama klabu nyingine yoyote.

“Lakini kuna jibu moja tu, kama nilivyowaeleza wachezaji wangu, kuna jibu moja tu – kufanya mazoezi kesho kwa ajili ya kujiandaa na mapambano yatakayotukabili mbele ya safari.

Audio: Mbowe akumbuka UKUTA, Asema Serikali inaendeshwa kwa hila
Antonio Conte Apangua Hoja Za Jose Mourinho