Kiungo kutoka nchini Ubelgiji na klabu ya Tottenham Hotspurs, Mousa Dembele yupo hatarini kufungiwa michezo kumi (10) na chama cha soka nchini England FA, endapo itathibithika alimfanyia utovu wa nidhamu kwa makusudi mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Diego Costa wakati wa mchezo wa ligi uliochezwa mwanzoni juma hili.

Dembele, ameonekana katika picha za televisheni za mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili, akimfinya sehemu za jicho la kushoto, Diego Costa baada ya kuibuka kwa malumbano baina ya wawili hao.

Chama cha soka nchini England FA, kwa sasa kinasubiri ripoti wa mwamuzi wa mchezo huo licha ya picha za televisheni kuanza kusambaa tangu jana katika mitandao ya kijamii, ambazo zinaonyesha matukio kadhaa ya utovu wa nidhamu yaliyokua yamekithiri katika mchezo huo.

Kifungo ambacho kiliwahi kumtia hatiani aliyewahi kuwa mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Luis Suarez baada ya kutuhumiwa kumng’ata kwa makusudi beki wa Chelsea Branislav Ivanovic, kinatarajiwa kutumika kwa Dembele.

Luis Suarez akimng’ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic, wakati alipokua akiitumikia Liverpool mwaka 2013

Suarez, baada ya kubainika alimng’ata kwa makusudi mkononi Ivanovic katika msimu wa 2012-13, aliadhibiwa kwa kufungiwa michezo kumi (10).

Pindi FA watakapoipata ripoti ya mwamuzi wa mchezo wa Chelsea dhidi ya Spurs, pia wataangaliza makossa mengine ya utovu wa nidhamu na huenda wageni katika mchezo huo wakaadhibiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuonyesha mchezo wa hovyo dhidi ya wachezaji wa The Blues.

Tanzia: Rais wa Zamani wa Burundi afariki
Serikali 'Yamfungia' Snura Na Chura Wake!