Meneja wa West Ham United, David Moyes, amesema kuwa anaweza kufundisha timu yoyote duniani na anataka kuonyesha kama ana uwezo huo akiwa na klabu hiyo.

Tangu ateuliwe kuwa mkufunzi wa wagonga nyundo wa London, ameisaidia timu hiyo kutoka katika mstari wa timu zinazotakiwa kushuka daraja na kuisaidia kutokufungwa michezo mitatu mfululizo.

“Nafikiri nina uwezo wa kufanya kazi hii katika klabu yoyote duniani na nina uhakika nitalifanya hili nikiwa na West Ham,” amesema Moyes

Aidha, Moyes mwenye miaka 54, anajaribu kurudisha heshima yake baada ya kufanya vibaya alipoviongoza vilabu vya Manchester United, Real Sociedad na Sunderland.

Hata hivyo, West Ham kwa sasa iko nafasi ya kumi na tano katika msimamo wa ligi ya nchini England.

Hijab yamponza muhitimu sheria
Bashe atuma salaam kwa makocha CCM