Ndege ya abiria ya Marekani iliyokuwa ikisafiri kutoka mji wa Seattle kuelekea Dallas nchini humo imelazimika kukatiza safari yake mara baada ya kugundulika kuwa kuna Moyo wa binadamu umesahaulika ndani ya ndege hiyo.

Shirika la ndege la Southwest limesema kuwa kiungo hicho cha binadamu kilisafirishwa Seattle kutoka California, ambako ilitarajiwa kutolewa baadhi ya mishipa ambayo ingetumiwa kwa tiba ya upandikizaji.

Lakini kisanduku ambacho kilikuwa kimehifadhi moyo huo kilisahaulika ndani ya ndege hiyo na hilo lilifahamika baada ya ndege kuanza safari kuelekea Dallas nchini humo.

Aidha, baadhi ya abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo walishtushwa na tkio hilo na walimtaka rubani wa ndege hiyo kurudi mara moja walikotoka ili waweze kuufikisha moyo huo sehemu ulipokusudiwa.

Hata hivyo, baada ya ndege hiyo kutua salama mjini Seattle, moyo huo ulipelekwa katika kituo cha afya cha kuhifadhiwa.

Antony Joshua ataja tarehe ya kuzichapa na Wilder
Fatma Karume anena kuhusu kufungua kesi dhidi ya Rais na AG

Comments

comments