Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amewataka wataalamu wa  Mipango na Maendeleo Vijijini kujiepusha na vitendo vya rushwa na ufisadi badala yake wafanye kazi zao kwa weledi ili kuwawezesha wananchi kujikwamua na umasikini.

Ameyasema hayo wakati wa mahafali ya 30 ya chuo cha Mipango na Maendeleo ya Jamii Vijijini kilichopo Dodoma ambapo amewataka wahitimu hao kuwa wabunifu na upangaji mzuri wa mipango ya maendeleo vijijini ambao utaharakisha nia ya Serikali  ya kuwaondolea wananchi umasikini.

“Ninawaasa wahitimu wetu muwe wazalendo na mkafanye kazi kwa bidii kokote mtakapo kwenda ili muwe kioo cha chuo hiki na Tanzania yetu inwataka muwe wabunifu na kukataa kujihusisha na mambo yanayo hatarisha amani’alisema Mpango.

Hata hivyo, Mpango amevishauri vyombo vya habari nchini kuandika habari kuhusu changamoto na fursa zinazowakabili wananchi vijijini.

Majaliwa amaliza mgogoro wa ardhi Manyara Ranch, Akabithi hati kwa Mkurugenzi
Diamond awataka mashabiki kumpa mtoto wake jina