Kongamano la siku tatu la kikanda kwaajili ya  hatua kuhusu ulemavu wa ngozi barani Afrika limehitimishwa leo  nchini Tanzania ambapo mpango huo utakua ni wa kwanza  kabisa kwa utekelezwaji kwaajiri ya kuzuia mauaji ya watu wenye Albino.

Mkutano huo  umefanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 17-19 juni  na uliandaliwa na mtaalam Huru kutoka Umoja wa Mataifa, Ikponwosa Ero na washirika wake na kuhudhuriwa na washiriki 150 kutoka nchi 29 za kanda ya Afrika.

Ikiwa ni pamoja na serikali ,na mashirika yasiyo ya kiserikali,taasisi za kitaifa za haki za kibinadamu,wanaharakati,wataalam wa haki  za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika pamoja na wasomi.

Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kutoa elimu  na kupunguza mashambulizi zidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kuuza viungo vyao vya mwili tabia inayoendelea barani afrika kutokana na ujinga  kuhusu chanzo cha kisayansi cha ulemavu wangozi,vitendo vya kishirikina na hatua zisizoridhisha za  zinazochukuliwa na serikali.

Aidha washiriki wate wa kongamano hilo waliitikia wito wa kutoa mapendekezo mazuri na kuandaa hatua maalum,rahisi na madhubuti ambazo zinaweza kutekelezwa na wadau wote ambazo ni hatua za kuzuia,kulinda,uwajibikaji nahatua za kupambana na ubaguzi.

Pia Tanzania imetajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino

Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino
Pamoja na juhudi ambazo serikali imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha Watanzania wenye ualbino wanakuwa salama na amani lakini bado Tanzania inaendelea kuwa nchi ya hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha unyanyasaji.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua kuhusu ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa kwa ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino.
“Tangu nimeingia sijawahi kufanya uchunguzi hata katika matokeo ya uchunguzi wa nchi 29 sijaujua sana lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nikipata kutoka kwa taasisi mbalimbali inaonyesha Tanzania ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa watu walio na uablino,” alisema Ero.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanguga alisema katika kongamano hilo wametoka na maazimio ambayo wanaiomba serikali iweze kuyafanya ili kuwezesha watu wenye ualbino kuwa na usalama wa uhakika.
“Tumejadili mambo mengi lakini tunaiomba serikali ihusike moja kwa moja kupinga unyanyasaji, ukatili na ubaguzi nia tunaiona kwahiyo tunaomba waendelee kuwa hivyo na pia waongeze bajeti na zaidi katika matibabu kwa watu wenye ualbino,” alisema Nyanduga..
Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia Mratibu Mkazi wa mashirika hayo, Alvaro Rodriguez alisema ni wataendelea kuwasaidia watu wenye ualbino ili kuwezesha kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.

Muigizaji maarufu Marekani ataka kumuabisha Trump na utajiri wake
Video: Bilioni 2.5 imetengewa Morogoro ujenzi wa Hospitali