Klabu ya Juventus imeonesha nia ya kutaka kumsajili tena kiungo wa klabu ya Manchester United Paul Pogba kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao msimu ujao wa ligi kuu Italia na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Juventus Mabingwa wa ligi kuu Italia imewasiliana na wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola juu ya kutaka huduma ya kiungo huyo Pogba mwenye umri wa miaka 26 raia wa Ufaransa.

Ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza Pogba alijiunga na klabu ya Juventus kwa uhamisho huru mwaka 2012, baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza klabu ya mpira ya Old Trafford.

Hata hivyo ,mchezaji huyo nyota alitumikia Juventus miaka minne kwa mafanikio makubwa kabla ya kujiunga tena na klabu ya Manchester United mwaka 2016 kwa kitita cha paundi milioni 89 kiasi ambacho kilivunja rekodi ya Dunia.

 

 

 

 

Kundi la waasi la ADF laua watu 12 DRC
Zitto asifu msimamo wa Serikali