Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi imeandaa
mpango maalumu wa upimaji wa Ardhi na Urasimishaji wa maeneo
yote
yasiyopimwa katika jiji la Dar es salaam ambapo viwanja
zaidi ya  laki tatu
(300,000) vitapimwa na wamiliki wake kupewa Hati.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam kuhusu zoezi hilo,
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Mozes
Kusiluka amesema
kuwa Serikali imeamua kuja na mpango huo kwa sababu ya
ukubwa wa jiji hilo
na wingi wa watu ulioambatana na ujenzi wa makazi holela.

“Katika mwaka wa fedha 2016/2017 tumepanga kuwa na mpango
maalum wa jiji la
Dar es salaam ambapo  wataalam wetu watakwenda,
> kuhakiki mipaka na kupima
maeneo yote ambayo hayajapimwa na kutengeneza ramani
zitakazoonyesha maeneo
ya barabara na maeneo ya huduma nyingine kwa kushirikiana na
wananchi
husika.

Amesema kuwa baada ya zoezi la uhakiki Serikali itatoa hati
za maeneo hayo
na kusisitiza kuwa zoezi hilo litafanyika pia katika maeneo
mengine ya miji
mikubwa nchini yenye watu wengi ikiwemo jiji la Mwanza.

Dkt. Kusiluka amesisitiza kuwa urasimishaji utakuwa
shirikishi kwa
kuwahusisha watu wote wa maeneo yatakayopimwa na Serikali
ambapo wananchi
wenye nyumba watashirikiana na viongozi wa Serikali katika
mitaa kupanga na
kuimarisha mindombinu ya maeneo yao pamoja na kukubaliana
maeneo ambayo
barabara za mitaa zitapita, mitaro ya maji machafu, magari
ya kupitishia
huduma za dharula kama Zimamoto nay ale ya kubebea
wagonjwa.

“Mpango wa urasimishaji ni Shirikishi, wataalam wa ardhi
watakwenda kwenye
> maeneo yote yatakayopimwa hususan katika jiji la Dar es
salaam na kukaa na
wananchi wote,kupitia mipaka wakishirikiana na wananchi wote
kwa uwazi ili
zoezi hilo liwe na manufaa na tija kwa wananchi wote”
Amesisitiza Dkt.
Kusiluka.

Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa sheria zinazoisimamia sekta
ya Ardhi
nchini Tanzania bado sekta hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali
ikiwemo migogoro ya Wakulima na wafugaji, migogoro ya
kijinai ya mtu mm
kuvunja nyumba au kuvamia eneo la mtu bila idhini, migogoro
ya mipaka kati
ya majirani na ile inayosababishwa na wananchi kutokujua
sheria.

Mbali na sababu hizo amebainisha kuwa idadi ya watu na
matumizi ya ardhi
kwa shughuli mbalimbali imekuwa ikiongezeka wakati ardhi
ikibakia ileile
jambo linaloifanya sekta hiyo kuja na mikakati mbalimbali ya
kukabiliana na
changamoto hizo kupitia watalaam waliopo.

Amesema kuwa serikali imefanya mambo mbalimbali kuhakikisha
kuwa inatatua
kero za wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali kwa
kuwatumia
wataalam wake kupima na kupanga maeneo ya vijiji mbalimbali,
kutoa elimu
pia kuajiri wataalam wa masuala ya Ardhi katika Halmashauri
zote nchini.

Aidha amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kupima maeneo
yote ya ardhi
nchini ambayo hayajapimwa kupitia mpango wa miaka 10.

Samia Suluhu;Wekeni Mipango Madhubuti Katika Upatikanaji Maji
Mashinji Awafunda Bavicha, Awapatia Mbinu za Kushinda 2020