Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema Tanzania imebaki kuwa miongoni mwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara Barani Afrika, ambazo uchumi wake unakua kwa kasi.

Dk. Mpango ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari , amesema kuwa ukuaji wa uchumi ni mojawapo ya vitu vinavyotazamwa katika kutathmini afya ya uchumi wa taifa.

“Tunaiona Tanzania imeendelea kufanya vizuri, uchumi unakua kwa kasi katika bara la Afrika, tunafanya majadiliano na Benki ya dunia na Umoja wa Ulaya kuhusu fedha za miradi ili tuweze kupiga hatua zaidi.”amesema Mpango.

Aidha Dk. Mpango amesema ustawi wa kukua kwa uchumi wa taifa unapimwa kwa kuangalia viashiria mbalimbali vikiwemo ukuaji wa pato la taifa, mfumuko wa bei, thamani ya shilingi, mwenendo wa sekta ya kibenki na sekta ya nje na akiba ya fedha za kigeni.

 

Makani: Faru John mwachieni Waziri Mkuu
JPM kushiriki mkesha mwaka mpya uwanja wa uhuru