Muigizaji maarufu duniani na star katika tamthilia ya power Rotimi ambaye kwa sasa kumekuwa na  tetesii za kutoka kimapenzi na Vanessa mdee, ameposti  mdogowake vanessa kupitia ukurasa wake wa instagram na kuandika  kuwa Mimi Mars (am proud of you) najivunia wewe ni baada ya mwanamuziki huyo kutajwa katika tuzo za kalasha Awards.

Mimi mars ambaye kwa sasa yupo chini ya lebal ya mdee music, tarehe 30 alikuwa akifanya uzinduzi ya filamu ya You again aliyoshiriki na  iliyooneshwa kwa mara ya kwanza Tanzania.

Mwanamuziki huyo na muigizaji, amechaguliwa kuwania tuzo ya Kalasha awards katika kipengele cha Best Acterss katika filamu aliyoigiza na waigizaji kutoka nchini Kenya inayoenda kwa jina la You Again.

Mimi mars ambaye aliwahi kuwa mtangazji na kuhamia katika tasnia ya muziki kwa sasa amijiingiza katika uigizaji huku akifanya vizuri na kuchaguliwa kuwania tuzo ambayo itamtambulisha vyema katika tasnia ya uigizaji.

Aidha mimi mars ametoa shukurani kwa wote waliojitokeza katika uzinduzi wa movie yake iliyooneshwa katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

 

 

 

Mfuga chatu maarufu auawa na chatu wake
Jinsi ya kutumia kabichi kama dawa

Comments

comments