Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amefanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es salaam ili kujionea utaratibu wa Bandari hiyo wa kuondosha taka zitokanazo na shughuli zake.

Ziara hiyo ya Mpina, imetokana na Malalamiko kutoka kwa wananchi yaliyodai kuwa uchafuzi mwingi unaofanyika Baharini na sehemu kubwa ya fukwe za bahari unasababishwa na shughuli mbalimbali zinazofanywa na bandari hiyo.

Aidha, Mpina amekagua maeneo ya kutoa na kukusanya taka za aina mbali mbali bandarini hapo zikiwemo taka za mafuta ghafi, pia kupokea taarifa kutoka kwa uongozi wa Bandari hiyo, ambapo ameshangazwa na kile kilicholezwa na Afisa Mazingira wa bandari hiyo, Thobias Sonda kuwa Bandani hiyo haina sehemu ya kupokea taka na wala haina takwimu zozote za taka zinazoingia na kutoka Bandarini hapo.

Kutokana na hali hiyo Mpina kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ameutaka uongozi wa Bandari hiyo kujenga mfumo mzuri wa kuhifadhi taka kwa muda wa miezi sita na kuripoti kwa Baraza la Mazingira kwa miezi mitatu Mfululizo kuonyesha namna ambavyo uondoshaji wa taka hizo unafanyika.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mamlaka ya bandari Tanzania,Nelson Mlele amesema kuwa  amepokea maagizo hayo kupitia NEMC kwani yanawakumbusha utekelezaji wa majukumu yao kwa upande wa Bandari ni changamoto itakayo fanyiwa kazi kwa haraka zaidi.

Hata hivyo  Afisa Mazingira wa bandari hiyo, Thobias Sonda amesema kuwa taka za maji taka pamoja na kukosekana kwa takwimu za uondoshwaji na umwagaji, taka hizo zimekuwa zikikusanywa na magari yao maalumu na kumwagwa katika mabwawa yaliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam.

Video: Mwakyembe avutiwa na kasi ya utendaji wa Makonda
Mapinduzi Cup - Azam FC Uso Kwa Macho Na Young SC