Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amekamata meli kutoka Malaysia ikiwa inavua samaki eneo la Tanzania la Bahari ya Hindi na kuitoza faini ya dola  350,000 ambayo ni sawa na Shilingi milioni 770 na kutaka fedha hizo zilipwe ndani ya siku 7.

Waziri Mpina amesema wameipa siku 7 badala ya saa 24 kwa sababu mmiliki wa meli hiyo hakuwepo.

”Sasa hawa wenzetu wamefanya hivyo, na imetangazwa faini hapa na mimi kama waziri nairidhia kabisa hiyo faini wanatakiwa wailipe mapema ndani ya muda uliotajwa” amesema Mpina.

Ameongezea kuwa Serikali haiwezi kuangalia madudu hayo yakifanyika na sheria za nchi zikivunjwa bila utaratibu wowote na kusema kuwa hali hiyo haiwezi kuvumilika watu hao lazima wawajibishwe vikali.

”Huu ni uharibufu wa hali ya juu ambao hauwezi kuvumilika, Kama Serikali lazima tuchukue hatua kali” amesema Mpina.

Aidha amewaomba watuhumiwa hao kufuata na kuzingatia sheria zilizowekwa na zinazowaongoza na sio kujifanyia tu mambo kama wanavyotaka.

 

 

 

 

JPM amlilia Mzee Kingunge
Marekani yamgeuzia kibao Odinga