Kero za Muungano ambazo zimekuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi zimepatiwa ufumbuzi kwa kiasi kikubwa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina alipokuwa akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wabunge.

Amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2006 hadi 2007 hoja 15 zilizowasilishwa kutafutiwa ufumbuzi kati ya hoja 11 zimepatiwa ufumbuzi.

“Serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kushughulikia kero hizo kadri zinavyojitokeza,”amesema Mpina.

Aidha, ametaja kero hizo kuwa ni pamoja na utekelezaji wa Sheria ya Tume za Haki za Binadamu na utawala Bora, Uvuvi kwenye ukanda wa bahari Kuu, ushiriki wa Zanzibar kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo, amezitaja kero zingine zilizopatiwa ufumbuzi ni ushiriki wa Zanzibar na Kampuni za Kimataifa, suala la ajira kwa raia wa Zanzibar, utafutaji na uchimbaji  wa mafuta na gesi asilia

Jamal Kisongo: Mbwana Samatta Ataondoka Ubelgiji
Real Madrid Wamuweka Njia Panda Manuel Neuer