Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametoa mwezi mmoja kwa maafisa wa serikali kuwasaka na kuwakamata watu wanaojihusisha na uingizaji wa mazao ya mifugo nchini kwa njia ya panya, ikiwemo maziwa na kuwachukulia hatua kali za kisheria ili kulinda uwekezaji mkubwa unaondelea kufanyika nchini.

Akizungumza katika kilele cha wiki ya maziwa yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma kwa njia ya kieletroniki, Waziri Mpina amesema Tanzania haiwezi tena kukubali kuwa soko la bidhaa zinazoingizwa kiholela kutoka nje.

Aidha amewaagiza wasindikaji na wanunuzi wa maziwa kuzingatia mwongozo uliotolewa na wizara ya kukununua maziwa ghafi kwa bei isiyopungua sh 800 kwa lita ya maziwa.

Hata hivyo Wizara hiyo imepokea maelekezo kutoka Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo,mifugo na maji, kupitia mwenyekiti wake Mahmoud Mgimwa ambapo ameitaka serikali kupiga marufuku matumizi ya maziwa ya unga katika ofisi za serikali.

Waziri Mpina amsema swala hilo litasimamiwa kikamilifu na wizara yake ili kuhamasisha viwanda vya ndani kuongeza uzalishaji.

Amewataka wazalishaji kote nchini kuongeza uzalishaji,kutumia fursa zinazotolewa na serikali na kuendelea kufuga ngombe wa maziwa kwa tija.

Uingereza: Sanamu ya mfanyabiasha wa utumwa yavunjwa kupinga ubaguzi
Simba SC yairarua Transit Camp