Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina ameliagiza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira NEMC kwa kushirikiana na uongozi wa kiwanda cha Azania kinachozalisha unga wa ngano, kupima kiwango cha ubora wa hewa inayoambatana na vumbi la unga wa ngano linalotoka kiwandani hapo.

Ameyasema hayo hii leo mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa amekuwa akipata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.

Amesema kuwa baada ya kuchukuliwa kwa vipimo hivyo na kutoa matokeo, Serikali ndiyo itajua hatua za kuchukua ili kuweza kumaliza tatizo hilo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi.

“Baada ya matokea hayo sasa serikali inaweza kuwa na nafasi ya moja kwa moja kuchukua hatua kwa mwenye kiwanda ikiwa ni pamoja na kukitoza faini kwa mujibu wa sheria, na kama matokeo ya vumbi na kelele zitokazo kiwandani hapo yatakuwa ndani ya kiwango, sasa hatua itakayofuata ni yakuangalia mahusiano kati ya mwenye kiwanda na wakazi majirani wa eneo hilo. amesema Mpina

Hata hivyo,, katika muendelezo wa ziara yake ya ufuatiliaji na utekelezaji wa sheria ya mazingira jijini Dar es Salaam, Mpina ametembelea kiwanda cha Chemi cotex  kilichopo Mbezi Beach.

Serikali yapewa masaa 72 kuishtaki IEBC
Video: Tyga avunja ukimya, aibuka na 'My Way'