Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imesema kuwa Taasisi ya Uhamiaji na Jeshi la Polisi ni muhimu katika ustawi wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira. Luhaga Mpina mara baada ya kufanya ziara visiwani Zanzibar ya kutembelea taasisi hizo huku akisema kuwa muungano huo unategemea sana amani.

Amesema kuwa ni lazima taasisi hizo kutembelewa mara kwa mara ili kuweza kuona namana ya kutatua changamoto zinazowakabili ili Serikali iweze kuzifanyia kazi na kuwawezesha kufanikisha majukumu yao vizuri.

“ Nataka niseme dhahiri kuwa taasisi hizi zinautendea haki Muungano kutokana na wao wenyewe wanavyotimiza majukukumu yao pamoja na changamoto zinazowakabili na kuiweka nchi katika utulivu na usalama.” Amesema Mpina.

Kwa upande wake Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Kamanda, Juma Yusuph Ali, amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto za kiusalama kisiwani humo kunahitajika juhudi na ushirikino wa pamoja kati ya wananchi, wadau na Jeshi la Polisi.

 

 

 

Video: Ruby afunguka nje ndani kuhusu mpenzi wake mpya, ujio wake mpya
Video: Misri yaleta neema ya viwanda nchini, Freemasons watoa tahadhari Tanzania