Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amesema Serikali ya awamu ya Tano inaongozwa na Nguvu za Mungu katika kuwatumikia wananchi wake na si vinginevyo.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Kusifu  na Kuabudu katika Kanisa la Tanzania Assemblies  of God lililopo  eneo la Kinzugi Salasala.

Aidha, amesema kuwa Serikali itaendelea kusimamia misingi yake bila kuogopa maneno ya watu wanaokatisha tamaa kwani Sheria na Katiba za nchi zinatokana na maneno yaliyopo  katika vitabu vya Mungu.

Hata hivyo, amewaomba watumishi wa Mungu kuenelea kuwaombea viongozi katika kutenda kazi zao kwani nafasi walizo nazo ni uchaguzi kutoka kwa Mungu na sio kwa nguvu za mtu yeyote.

“Utawala wa awamu ya tano tunamtanguliza Mungu mbele,tunaomba muendelee kutuombea tutekeleze majukumu yetu licha ya kuwepo kwa vikwazo mbalimbali katika kutekeleza majukumu yetu,”alisema Mpina

Aidha aliziomba familia za kikristo na jamii kwa ujumla kuwa mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira kwani bila kuwepo kwa mazingira safi magonjwa yatapata nafasi katika jamii.

Kwa Upande wake,Mchungaji wa Kanisa la Assembly of God ,Deusi Sabuni alisema  watahakikisha wanaendele kufanya Maombi kuiombea Serikali ya awamu ya tano na viongozi wake.

Mtoto darasa la tano ajitia kitanzi bafuni.
Dangote aipaisha Tanzania kimataifa