Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkabidhi mpira Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga ikiwa ni ishara ya Naibu Waziri huyo kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yajulikanayo kwa jina la Mpinga CUP yanatarajiwa kuanza kesho jijini humo.

Katika hotuba yake, Masauni aliwataka waendesha Boda Boda jijini humo na nchini kwa ujumla kufuata sheria za usalama barabarani, na pia elimu ambayo wanapewa waitumie vizuri ili kuepuka ajali mbalimbali zinazosababishwa na uzembe wa madereva hao

Video: Majambazi hatari wanne wakamatwa Dar es salaam
Wahandisi Watakiwa Kuandaa Kampeni Mbalimbali Mashuleni Kuhamasisha Watoto Wa Kike Kusoma Masomo Ya Sayansi