Chama tawala nchini Angola, MPLA kimedai kuwa kimeshinda kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, wakati ambapo tayari kura milioni tano zimekwisha hesabiwa na kufanya njia nyeupe kwa waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Jouao Lourenco.

Waziri huyo wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, Jouao Lourenco anatarajia kupokea kijiti kutoka kwa Rais wa sasa, Jose Eduardo dos Santos aliyetawala nchi kwa muda wa miaka 38

Aidha, Chama cha MPLA kimesema kuwa kimeshinda uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumatano baada ya kupitia taarifa kutoka kwa mawakala wake walio kwenye vituo mbalimbali kote nchini humo.

Hata hivyo, Ripoti hiyo imekuja wakati chama kikuu cha upinzani, UNITA, kikituhumu kwamba jeshi la polisi nchini humo lilifyatua risasi na kuwakamata baadhi ya wafuasi wa chama cha upinzani katika baadhi ya vituo vya kupigia kura wakati wakiendelea kupiga kura katika mji wa Huambo.

Video: Ndugai atoboa siri Maalim Seif kukwama, Mkemia mkuu kitanzini
Prof. Mkumbo azifunda mamlaka za maji