Mwanamuziki wa nyimbo za asili nchini, Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba ambaye kwa sasa anatamba na kibao cha ”Nimwage Radhi” alichofanya na msanii toka kundi la WCB, Harmonize amesema anatamani uhasama uliopo kati ya Diamond Platinumz na Ali Kiba uendelee kuwepo daima.

Mpoto amesema uhasama wao umekuwa na manufaa katika muziki wa Bongo Fleva na burudani kwa ujumla na kwamba anaona wakipatana watapoteza ladha ya muziki huo wa Tanzania unaokuja juu.

”Yaani mwenzenu hilo bifu la Diamond na Kiba nalifurahia sana, limeleta utamu katika muziki ninachoomba tu libaki katika soko la muziki na lisiwe lile la kushindwa hata kusalimiana” amesema Mpoto.

Mpaka leo naamini wanaowatengenezea uadui ni mashabiki wa muziki wao kitu ambacho ni kizuri kinachowasaidia katika muziki wao.

Mpoto ameongezea kuwa haoni sababu ya wawili hao kutoa nyimbo pamoja kwa kuwa wataharibu utamu mzima na ushindani wao na kutaka wabaki hivyo hivyo.

Toa maoni yako juu ya mtazamo wa Mrisho Mpoto wako.

 

Wema Sepetu kufanyiwa upasuaji India
LIVE: Misa ya Kuagwa kwa Marehemu Bilago Bungeni Jijini Dodoma