Mrisho Mpoto amemuandikia Diamond Platinumz ujumbe wa ushauri akimkumbusha kuhusu msiba wa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Mpoto ambaye ni rafiki wa Diamond kwenye biashara ya muziki, ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akitoa wito kwa msanii huyo kama kaka yake anayemheshimu.

Ameweka picha ya Diamond ambayo aliipost hivi karibuni na kuandika, “Nasib Abdul nimekuita kwa jina lako la kuzaliwa mimi kama kaka yako unaeniheshimu na kunisikiliza nakwambia RUGE MUTAHABA AMEFARIKI nakuomba NJOO UMZIKE.. nimemaliza.”

Wito huo wa Mpoto umekuja wakati ambapo Diamond amekuwa akikosolewa kwenye mitandao ya kijamii kwa kutoonesha kujihusisha na msiba wa Ruge.

Ruge na Diamond walifanya kazi nyingi pamoja, na alihusika katika kuiandaa show kubwa zaidi ya kwanza ya msanii huyo ‘Diamonds are Forever’ ambayo ilihudhuriwa kwa kiingilio kikubwa zaidi kuwahi kutokea wakati huo.

Hata hivyo, katika miaka miwili iliyopita Diamond na Marehemu walilipotiwa kuwa katika kipindi cha kutofautiana.

Video: Ukaguzi wa maduka ya fedha watikisa Dar, Maelfu ya Walimu kuajiriwa nchini
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 1, 2019

Comments

comments