Mabingwa wa Soka wa DR Congo na klabu mwalikwa kwenye michuano ya ‘Simba Super Cup’ TP Mazembe wametangaza kikosi kitakachoshiriki michuano hiyo, itakayoanza rasmi keshokutwa Jumatano (Januari 27), jijini Dar es salaam.

Kwenye kikosi cha TP Mazembe kilichoanikwa hadharani tayari kwa safari ya kuja Tanzania, yupo mshambuliaji mkongwe Tresor Mabi Mputu sanjari na mshambuliaji Mtanzania Thomas Ulimwengu.

Hata hivyo baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo yenye mskani yake makuu mjini Lubumbashi, hawatokua sehemu ya safari ya kuja Tanzania, kufautia kukabiliwa na majukumu ya timu ya taifa kwenye Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’ zinazoendelea nchini Cameroon.

Kwenye michuano ya Simba Super Cup, TP Mazembe wataanza kupambana dhidi ya El Hilal ya Sudan Januari 29 na kisha watakiputa dhidi ya wenyeji Simba SC Januari 31, ambao wataanza michuano hiyo dhidi ya El Hilal Januari 27, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Rais wa Ethiopia awasili nchini
Zanzibar kuja na mpango wa kuboresha utalii