Msanii Mr Blue amefunguka na kusema kuwa yeye alianza muziki kwa kuiba ‘verse’ ya mtu kipindi alichokuwa mdogo na hivyo alipoimba na kupata shangwe sana kwa watu ndiyo kitu kilichomsukuma kufanya muziki

Mr Blue amesema kuwa yeye hakuwa na mpango wa kuwa msanii lakini alivyo hama na kuenda manzese hapo ndipo alipoanza kujihusisha na masuala ya muziki.

“Kwa hiyo nilipohamia huko ndiko kulikuwa nyumba ya muziki, nikajikuta nawasikiliza sana na kukariri ‘verse’ hivyo kuna siku nilikwenda sehemu na kuchana verse ya mtu nilishangiliwa sana, kwa hiyo mimi naweza kusema nimeingia kwenye muziki kwa kuiba ‘verse’ ya mtu ambaye naye nilimkuta huko nilikohamia” amesema Mr Blue.

Hata Hivyo, Mr Blue amesema kuwa katika maisha yake ya muziki amekosa mengi ambayo alikuwa anastahili kuyapata kwenye muziki wake kama tuzo mbalimbali na jasho lake kwenye album zake alizotoa kipindi cha nyuma kwani hakunufaika nazo.

Serikali yasitisha mnada wa Tanzanite
Sheikh Ponda atii amri ya RPC Mambosasa

Comments

comments