Waziri wa Maji Juma Aweso, akiwa mkoani Mtwara na kutembelea kwa kushtukiza mradi mkubwa wa Chujio la Maji (Rapid Sand Filter)uliopo Mangamba, kujionea ujenzi unaoendelea chini ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara (MTUWASA).

“Chujio hili ni muhimu sana na ni hatua ya kihistoria kuelekea upatikanaji wa Maji safi na salama kwa wana Mtwara,” Amesema Waziri Aweso
Waziri wa Maji Juma Aweso akisaidia kuchota zege katika mradi mkubwa wa Chujio la Maji (Rapid Sand Filter) ulio chini ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara (MTUWASA).
Aidha mradi huo upo katika hatua za mwisho za ujenzi na unatarajiwa kumalizika ifikapo mwezi Septemba 2021.
Waziri wa Maji Juma Aweso akitoa maelekezo kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara (MTUWASA) ambao ndio wasimamizi wa mradi huo.
Aidha Waziri Aweso ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa (MTUWASA) ili kuhakikisha wakazi wa Mtwara wanapata Maji Safi na salama mara baada ya Chujio hili kukamilika.
Waziri wa Maji Juma Aweso akipokea maelekzo kuhusiana na mradi na kujionea hali ya mradi unavyoendelea huku akiridhishwa na hatua ya mradi ulipofikia.
Azam FC yatema maproo wanne
Bashungwa atoa maagizo kwa maafisa michezo