Taasisi ya Huduma za afya Aga Khan Tanzania, wamesaini na kuzindua mradi wa kuboresha matibabu ya dharura nchini Tanzania (IMECT), ambao unaweka mkazo katika kuimarisha miundombinu kwa kutoa vifaa vya matibabu ya haraka kwenye vituo vya afya, sekta za umma na binafsi.

Mratibu Mkuu wa huduma za dharura za matibabu ya wagonjwa mahututi, usimamizi wa kesi za mlipuko na maafa, Dkt. Erasto Sylvanus akizungumzia hatua hiyo amesema, Hospitali zinazotoa matibabu ya haraka, baadhi yao hazina usimamizi wa matibabu ya haraka na zina upungufu wa wafanyakazi wenye mafunzo sahihi ya dharura .

Amesema, “Suala la magonjwa yasiyoambukiza linazidi kuongezeka huku kisukari, shinikizo la juu la damu na majeraha ya ajali za magari zikiwa sehemu kubwa ya ongezeko hilo, na katika hospitali zinazotoa huduma za haraka nyingi zina upungufu wa wafanyakazi.”

Awali, Mkuu wa Idara ya dharura kutoka Taasisi ya huduma za Aga Khan Tanzanzia, Dkt. Sherin Kassamali amesema mradi huo unatarajia kuwapa mafunzo wafanyakazi 120 wa mstari wa mbele katika dharura ya ajali , wafanyakazi 1000 wa afya katika kutoa matibabu bora ya dharura na wafanyakazi 60 wa afya kuwa wakufunzi.

Kwa upande wake, Balozi wa Poland nchini, Krzysztof Buzalski amesema “Mradi huu utatekelezwa na kituo cha kimataifa cha misaada cha Poland, moja ya mashirika makubwa zaidi na ya kiweledi zaidi yasiyo ya kiserikali ya poland yenye uzoefu mkubwa katika afya , matibabu ya dharura na kuokoa maisha ya ulimwenguni na katika kanda hii.”

Mradi huo wa miaka miwili na miezi minne, utakaogharimu shilingi 1.8 Bilioni utafanyika kati ya Taasisi ya huduma za afya Aga Khan Tanzanzia, serikali ya Poland na kituo cha kimataifa cha misaada cha Poland watakaotoa mafunzo kwa wakufunzi na watoa huduma ili kuendeleza stadi katika utoaji wa matibabu ya dharura nchini.

Gadiel Michael afungiwa Michezo mitatu
Mwinyi Zahera Kocha mpya Polisi Tanzania FC