Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo amesema kuwa ameridhishwa na jitihada zinazofanywa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), katika kuhakikisha Miradi hiyo inakamilika kwa wakati, ambapo mpaka sasa ujenzi wa mradi wa kinyerezi II umefikia asilimia 53%.

Amesema hayo Jijini Dar es salaam wakati wa Ziara yake katika Miradi ya kuzalisha umeme wa Gesi Asilia na upanuzi wa Kinyerezi I na II.

Amesema kuwa maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Kinyerezi II, unaendelea vizuri na unatarajia kukamilika Desemba 2018, ambapo mpaka sasa mradi huo unategemea Kinyerezi I kutokana na baadhi ya mitambo kuingiliana.

“Niwapongeze sana TANESCO kwa jitihada kubwa mnazozifanya katika kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati, ambapo mmewezesha jenereta 8 zenye jumla ya Megawati (MW) 240
mpaka sasa zimeshafika, hii  ni hatua nyingine kubwa sana ,hivyo  kupitia Mradi huu wa kinyerezi nina amini Tanzania ya Viwanda inawezekana”, amesema Dkt. Pallangyo.

Kwa upande wake Meneja wa Kituo cha Kinyerezi II, Mhandisi Steven Manda amesema kuwa kituo hicho kinaendelea vizuri na ujenzi ili kuhakikisha kinakamilika Desemba 2018.

Naye Kaimu Meneja wa Kituo cha Kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge amesema kuwa Mradi
huo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 150, Umeongezewa uwezo wa kuzalisha Megawati
zingine 185 ikiwa ni Awamu ya pili ya upanuzi wa mradi huo.

Hata hivyo, Mhandisi Busunge ameongeza kuwa miradi hiyo miwili kwa ujumla miradi yote itakapokamilika,itazalisha jumla ya Megawati 575 za umeme utokanao na Gesi Asilia.

Video: Kendrick Lamar na Eminem ‘Washindanishwa’, Mijadala Yateka Vituo
Mahakama Yamuachia Huru Mtuhumiwa Wa Richmond