Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party Augostino Lyatonga  Mrema , amewapongeza wabunge  wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kwa maamuzi yao ya kuhudhuria vikao vyote vya bunge.

Mrema amesema kuwa bunge ni mhimili nyeti wa serikali hivyo kuwa na wabunge wa upande mmoja si sahihi kwa sababu wabunge wote wamechaguliwa na wananchi ambao ni wapiga kura wao, hivyo kususia bunge ni kuwanyima haki wapiga kura wao.

Aidha Mrema aliongeza kuwa uwepo wa wabunge wa upinzani bungeni kunaleta changamoto kubwa na kuboresha bunge kwa kuchangia mijadala mbalimbali kwa lengo la kuisadia serikali katika suala zima la kuleta maendeleo.

”Haikuwa busara kwa wabunge wa upinzani kususia vikao vya bunge kwa sababu kufanya hivyo ni kuwanyima haki wapiga kura wao”alisema mrema kwenye barua aliyomuandikia spika wa bunge.

Shimon Perez Akimbizwa Hospitalini
Zanzibar Queens Yaendelea Kuwa Mdebwedo