Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party Taifa (TLP), Augustino Mrema amesema kuwa hatomvumilia wala kuruhusu mtu yeyote kumchezea Rais Dkt. John Magufuli.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo ametoa wito kwa Watanzania kumlinda na kumsaidia Rais Magufuli katika majukumu yake ya kuiongoza nchi.

“Sitaruhusu mtu yeyote amchezee Rais Dkt. Magufuli, sitaki ujinga ujinga huo ufanyike kama ilivyozoeleka kwa baadhi ya wanasiasa kumtolea lugha chafu,” amesema Mrema.

Aidha, katika hatua nyingine, Mrema amewashauri wanasiasa kuacha siasa za maji taka hasa zenye nia ya kumkshifu Rais Magufuli badala yake wamsaidie.

Hata hivyo Mrema ameongeza kuwa kuongoza nchi kama Tanzania ni ngumu sana, hivyo cha msingi amewaomba wananchi na wanasiasa kumsaidia Rais Dkt. Magufuli na si kumtolea lugha chafu.

 

 

Leonardo amkataa Antonio Conte AC Milan
Dkt. Bashiru aikana kauli yake, adai Bashe, Nape sio watukutu