Mwanasiasa Mkongwe, Augustine Mrema amemuelezea Rais John Magufuli kama kiongozi wa Tanzania anayetenda miujiza kutokana na utendaji wake ndani ya siku 100 tangu alipoingia madarakani.

Mrema ambaye alikuwa mbunge wa zamani jimbo la Vunjo na kuangushwa kwenye uchaguzi uliopita na James Mbatia (NCCR – Mageuzi), aliendelea kuutetea uamuzi wake wa kumpigia debe Dk. Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ingawa chama chake cha TLP kilikuwa kimesimamisha mgombea urais.

“Nilijua wazi Rais Magufuli ni mtendaji ndio maana hata wananchi waliponiadhibu kwa sababu ya kumpigia debe sikuumia, najivunia chaguo langu na kiukweli anafanya miujiza ya hali ya juu,” alisema Mrema.

Mrema ambaye ni mwenyekiti wa TLP, alimuelezea Magufuli kama kiongozi mwenye uthubutu huku akiwataka watanzani kuacha unafiki na kumpa nafasi zaidi ya kufanya kazi.

 

BEN POL NA JUX WAPEANA MAKAVU KWENYE 'NAKUCHANA', usikilize hapa
Kanye West aomba msaada, atangaza kuzidiwa na madeni