Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa hama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema amesema kuwa yeye ni mzima wa afya.

Mrema amesema hayo baada ya kusambaa taarifa mitandaoni zikidai kuwa amefariki dunia akiwa nchini Afrika Kusini.

“… nimeanza kupokea salamu za pole, wengine Watanzania wakienda nyumbani kwangu, wakienda kijijini kwetu Moshi. Nachopenda kuwathibitishia mimi siumwi,” ameeleza Mrema kwenye taarifa yake kwa umma.

Ameongeza kuwa hajasafiri kwenda Afrika Kusini na kwamba mara ya mwisho kutoka nje ya nchi ilikuwa mwaka 2020.

Wananchi wazuiwa kuchukua mchanga wa kaburi la Maalim Seif
Masharti magumu kambini Young Africans