Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema amesema kuwa UKAWA hawampendi wala hawamtaki ndiyo maaana walifanya kila namna kuhakikisha wanampokonya Jimbo la Vunjo kwa kumsimamisha James Mbatia katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Ameyasema hayo kwenye kampeni za kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia chama cha TLP, Dkt. Godfrey Malisa na kusema kuwa wapinzani nchi hii wamekuwa wakimchukia.

“Ni kweli kwamba UKAWA hawanipendi, hawanitaki wakaninyang’anya lile jimbo wakampa James Mbatia angekuwa basi anafanya kazi za wananchi wa Vunjo wala nisingelalamika. Angelikuwa mwaminifu kwa Rais wetu wala nisingehangaika wala kulalamika, lakini walininyang’anya jimbo kwa ulaghai na utapeli kwa maneno ili kunimaliza kwa wananchi wa Vunjo wakasema Mrema ni mzee na kweli ni mzee ila kuwa mzee siyo kosa wala siyo dhambi kwamba wazee hawana manufaa,”amesema Mrema

Hata hivyo, Mrema amesema kuwa UKAWA wanamuita marehemu mtarajiwa hivyo amewataka kuacha tabia hiyo mara moja kwani wakiendelea hawatapata kura za wazee nchi nzima.

 

Video: Familia yakuna kichwa mazishi ya Kingunge, Zitto Kabwe 'ajivisha mabomu'
Magazeti ya tanzania leo Februari 3, 2018

Comments

comments