Mwenyekiti wa Taifa chama cha Tanzania Labour Party  ( TLP), Augustino Mrema amewataka wananchi wa Zanzibar kutoyumbishwa na kauli za wanasiasa ambazo zina lengo ya kuvuruga amani ya nchi kwa ujumla.

Mrema amezungumza hayo leo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari na kusema kwamba amani ya Zanzibar ni muhimu kuliko maslahi binafsi hivyo ni vyema kuzitafakari kauli ambazo zinaweza kuleta machafuko.

Amesema hakuna mtu aliye  juu  ya sheria hivyo kuwepo kwa watu wanaochochea  vurugu  ni kama waahini pia ni  vyema  hatua zichukuliwe dhidi yao katika kuhakikisha  wanachi wanakuwa salama

Aidha Mrema amesema kwamba amani ya Zanzibar ikiharibika hata bara haiwezi kuwa salama hivyo ni vyema kauli za kuvuruga amani zizingatiwe ili kulinda maslahi ya wananchi wa pande zote mbili.

Hata hivyo amesema Zanzibar ina historia ya kuuawa watu mwaka 2001kutokana na vurugu za kisiasa hivyo lazma  kwa  sasa suala la ki uchochezi liangaliwe kwa macho mawili dhidi ya watu wanaotaka kuvuruga amani katika mazingira hayo.

Mrema amesisitiza hakuna chama cha siasa ambacho  kinajengwa kwa kususia uchaguzi bali kwa kufanya hivyo ni  kuwanyima wapiga kura haki pi ni hatari na  kunaweza kusababisha chama kusambaratika kama kulivyotokea kwa baadhi ya vyama mfano, UPC cha Uganda na vinginevyo.

Pamoja na hayo mrema amefafanua kwamba mahakama ya ICC haingalii tu viongozi wa serikali bali hata viongozi wa kisiasa ambao wamesababisha mauaji kutokana na kauli wanazozitoa.

Pia mwenyekiti huyo wa TLP amewataka wahisani kutoingilia mambo ya ndani ya nchi kwani kusitisha misaada kwa hoja ya kufutwa uchaguzi wa Zanzibar na sheria ya mitandao ni kuingilia uhuru wa watanzania.

Video: 'Kama Watanzania Wengine Wameogopa Kusema mimi Nitasema' - Mrema
CAF Wamteua Michael Richard Wambura