Msichana mmoja mrembo raia wa Jamhuri ya Czech amepoteza maisha kwa ajali ya gari akiwa anajichukua video na kuirusha mubashara kwenye mtandao wa Facebook (Facebook Live).

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Czech, msichana huyo aliyetajwa kwa jina la Nikol Barabasova alikuwa abiria kwenye gari la rafiki zake, ambapo alianza kuchukua video ya safari yao mubashara kwa kutumia simu yake ya mkononi hadi walipopata ajali mbaya.

Video iliyochukuliwa na mrembo huyo imeonekana Facebook ambapo gari lao liligonga kingo za barabara na kusababisha kifo chake.

Kamera ya simu hiyo ilirekodi matukio ya purukushani za ajali hadi ilipofikia mwisho ikaonesha mkanda wa gari pekee huku kukiwa na utulivu, hakuna kilichokuwa kikitembea tena.

Imeripotiwa kuwa rafiki wa Nikol aliyekuwa kwenye gari hilo pia alikimbizwa hospitalini akiwa katika hali mbaya na kulazwa katika chumba cha mahututi (ICU) akiwa na jeraha kubwa kichwani.

Panga lafyeka mshahara wa Rais, wabunge Kenya
Video: Mbowe azumgumza baada ya Mdee kuachiwa kwa dhamana