Hatimaye mshindi wa mashindano ya kumsaka Mrimbwende wa Dunia, Miss World 2018 ametangazwa leo kuwa ni mrembo kutoka Mexico, Vanessa Ponce, lakini Afrika imebebwa na mrembo wa Uganda, Quiin Abenakyo aliyetinga tano bora.

Vanessa Ponce, Miss World 2018

Abenakyo, ameibuka kuwa mshindi wa taji la Miss World Africa, akishika nafasi tano za juu zaidi katika mashindano hayo ya 68, hatua mbayo haijawahi kufikiwa na mwakilishi wa Uganda tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 1951.

Abenakyo amefuata nyayo za mrembo wa Tanzania, Nancy Sumari aliyenyakua taji hilo la Malkia wa Afrika (Miss World Africa) mwaka 2005. Kama ilivyo kwa Abenakyo, Nancy alikuwa Mtanzania wa kwanza kufika hatua hiyo tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.

Nancy Sumari

Mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya mwaka huu, Queen Elizabeth Makune pia amefanya vizuri akiingia kwenye kinyang’anyiro cha warimbwende 100 waliokuwa na nafasi ya kutwaa taji la dunia. Hata hivyo, bahati haikuwa kwake, licha ya kuonekana kukubalika na wengi kupitia kura alizokuwa amepigiwa kura hizo hazikutosha kwenye mchakato huo pamoja na vigezo vingine.

Queen Elizabeth Makune, Miss Tanzania 2018

Mexico imeandika historia ya kuchukua taji la Miss World kwa mara ya kwanza, huku nafasi ya pili ikienda kwa mrembo wa Thailand, Nicolene Limsnukan. Nafasi tatu za kukamilisha nafasi tano za juu zilienda kwa Uganda, Jamaica na Belarus.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 9, 2018
Korosho zote zitabanguliwa nchini - Waziri Hasunga