Mtunzi na mwimbaji nguli wa ngano za Kiswahili zilizoshiba, Mrisho Mpoto ameeleza kuguswa na nyimbo za rapa Nay wa Mitego ambaye wiki hii alikumbwa dhahma ya kufungiwa kufanya muziki na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kipindi kisichojulikana.

BASATA walitangaza kumfungia Nay wa Mitego kwa kile walichoeleza kukiuka maadili ya kitanzania katika nyimbo zake licha kupewa onyo mara kadhaa. Wimbo ulioamsha hasira zaidi kwa BASATA ni ‘Pale Kati Patamu’ ambao hata hivyo waliufungia muda mfupi baada ya kutoka.

Nay wa Mitego

Mrisho Mpoto ametumia ukurasa wake wa Instagram kueleza kilicho moyoni mwake wakati alipokuwa akisikiliza nyimbo kadhaa za rapa huyo mwenye mashairi tata, akieleza kukunwa na uwezo wake.

Ingawa Mpoto ameonesha kutoelewa undani wa sakata la kufungiwa kwa Nay wa Mitego, amesemshauri kuzihariri nyimbo zake sehemu zenye ukakasi.

“Hapa nasikiliza nyimbo ya @naytrueboy hivi nyimbo gani imefungiwa? au yeye ndiyo kafungiwa? naomba mnielekeze nikamuone onetime, huyu mtu hatari sana si aedit tu ile sehemu!!” Ameandika Mpoto kwenye picha inayomuonesha akiwa na ‘headphones’.

Waziri Mkuu Aitaka Halmashauli Ya Temeke Kuondoa Wafanyakazi Wa Mkataba
Kigwangala Akutana Na Viongozi Wa Mfuko Wa Abbot