Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa ameyaomba mataifa ya Magharibi kuiondolea nchi hiyo vikwazo bila masharti yoyote ili kuuokoa uchumi wake ulioporomoka.

Amesema kuwa vikwazo hivyo ni kigezo kikubwa cha kukwamisha shughuli za maendeleo za Zimbabwe kwa miaka mingi.

Nchi za Magharibi ziliiwekea vikwazo Zimbabwe iliyokuwa inaongozwa na Robert Mugabe kutokana na sababu mbalimbali mojawapo ikiwa kuminya demokrasia na kutaifisha mashamba yaliyokuwa yanamilikiwa na raia wa nchi za Magharibi.

Katika hatua nyingine, Mnangagwa ambaye alikuwa anahutubia kikao cha viongozi wa Zanu-PF alisema kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi Julai mwakani unaweza kufanyika mapema zaidi.

Alisema kuwa Serikali yake itahakikisha uchaguzi huo unakuwa huru na haki.

Mnangagwa alikuwa Rais wa Zimbabwe mwezi uliopita baada ya Mugabe kulazimika kujiuzulu.

Ratiba mpya ligi kuu Tanzania bara
Video: Kama vyuma vimekaza wekeni grisi- JPM, Mwaka 2017 wapinzani wamevugwa