Jimbo la Arumeru Mashariki tayari limepata mbunge kutoka Chama Cha Mapinduzi CCM ambaye ametangazwa kupita bila kupingwa baada ya wagombea wenzake 10 kutokidhi vigezo.

John Palangyo amechukua nafasi ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Joshua Nassari wa Chadema ambaye alivuliwa ubunge huo.

Hapo awali Palangyo alikuwa mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa Kamati ndogo ya Uchumi, fedha na Uwekezaji.

Akizungumza, Palangyo amesema kuwa Jimbo la Arumeru limeteseka sana hasa upande wa barabara hivyo ameahidi kuhakikisha barabara zinajengwa.

”Kwakweli jimbo hili limeteseka sana naahidi nna kerwa kuna mambo yananikera kuna maji, umeme, barabara na zaidi sana barabara jimbo letu halina barabara kabisa nitajitahidi kuhakikisha kwamba barabara zinatengenezeka” amesema Palangyo.

Aidha amekumbusha kufuatilia ahadi ya Rais Magufuli aliyoitoa kipindi cha uchaguzi 2015 ya kuwapatia eneo la kilomita tano amesema wakati umefika kufuatilia ahadi hiyo.

Nassari ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo alivuliwa ubunge na spika wa Bunge Job Ndugai kwa kosa la utoro wa kutohudhuria vikao vya bunge vitatu mfululizo bila kutoa taarifa hali iliyoleta tafsiri kuwa amejivua sifa za kuwa mbunge.

Nassari katika utetezi wake alisema hakuhudhuria vikao hivyo alikuwa nje ya nchi akimuuguza mke wake.

Video: Tazama maana ya neno "MISSED CALL" ? / Walivyotamka neno "CHARACTERISTIC" ??
Dkt. Bashiru azungumzia mjadala wa Katiba Mpya wa bungeni