Baada ya Zinedine Zidane kutangaza kujiuzulu nafasi ya ukocha wa klabu ya Real Madrid majina mbalimbali ya makocha yamekuwa yakitajwa kuchukua nafasi ya Zizou ambaye amepata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi akiwa na matajiri hao wa Santiago Bernabeu.

Kocha wa klabu ya Tottenham, Mauricio Pochettino anatajwa kuwa moja kati ya makocha wanaopewa kipaumbele kumrithi Zidane licha ya kocha huyo raia wa Argentina kusaini mkataba mpya wa maiaka mitano kuendelea kubaki Tottenham.

Pochettino mwenye umri wa miaka 46 anaaminika kwa kufundisha mpira wa kuvutia na ameiwezesha Tottenham kumaliza ligi katika nafasi nne za juu misimu mitatu mfurulizo akiwa na kikosi cha wachezaji ambao sio wa garama kubwa.

Arsene Wenger amekuwa akitajwa mara kadhaa kutakiwa na Real Madrid siku za nyuma ingawa mashabiki wengi wa soka wamekuwa na mtazamo tofauti wengine wakienda mbali na kusema Wenger kwenda Madrid ni kumaanisha Madrid wasishinde vikombe kwa miaka kumi.

Gazeti la ‘Sun’ limeripoti kuwa Madrid wanamtaka pia kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amaye aliiongoza klabu hiyo kufika fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya.

Tumeshuhudia machocha wengi wakifukuzwa Real Madrid kutokana na bosi wa klabu hiyo Florentino Perez kuwa mtu anayependa mafanikio ya haraka, anapenda kuona timu ikishinda vikombe jambo amablo Zidane amelifanikisha ndani ya muda mfupi, swali je ni kocha gani ambaye ataweza kufikia mafanikio hayo au kumridhisha Perezi?.

 

Video: Nchi zilizovunja rekodi kuchukua kombe la dunia mara nyingi zaidi
Mahakama ya Uswiz yamtoa kifungoni Paolo Guerrero