Taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema kuwa kumekuwa na matukio makubwa ya uvunjifu wa amani ambayo yameyumbisha juhudi zote za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola huko Butembo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Kwa mujibu wa msemaji wa UN, Farhan Haq wakati operesheni zikiwa zimezinduliwa upya, WHO inamatumaini kwamba harakati za kuchukua vipimo katika maabara ambazo bado zinakabiliwa na vizuizi, vitapelekea kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wenye virusi vya Ebola katika siku zijazo.

Mlipuko huo uko katika hatua hatarishi, ambako kunaongezeko kubwa la maambukizi katika wiki za hivi karibuni jambo ambalo linahatarisha kuenea kwa maambukizi hayo katika majimbo mengine nchini humo.

Aidha, WHO imesema kuwa kunahitajika msukumo mkubwa wa msaada wa kisiasa na kifedha kutoka kwa wahusika nchini DRC na Kimataifa kukabiliana na hali hiyo tata.

Hata hivyo, hadi Mei 2, WHO ilikuwa tayari imepokea dola za Marekani milioni 32.5 zilizokuwa zinahitajika kuendeleza juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo kwa kiwango kilichofikiwa hivi sasa.

 

Waasi nchini Yemen kusitisha mapigano
Marekani yapandisha ushuru kwa bidhaa kutoka China