Rais John Magufuli, leo amelazimika kusimama na kuwasalimia wananchi katika eneo la Msamvu Mjini Morogoro baada ya wananchi hao kuusimamisha msafara wake ili wasikie neno kutoka kwa Mkuu huyo wa nchi aliyekuwa akisafiri kwa gari kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Akiongea na wananchi hao, Rais Magufuli amewataka watu wote ambao serikali iliwauzia viwanda na mashamba kuhakikisha wanaviendeleza haraka vinginevyo Serikali itawanyang’anya na kuwapa watu wengine.

Rais Magufuli ameeleza kuwa agizo hilo ni kwa wamiliki wote wa mashamba na viwanda visivyoendelezwa bila kujali itikadi zao za vyama.

“Wale wanaovimili hivyo viwanda, wawe wa CCM, wawe Chadema na  hata kama hawana vyama, lazima waviendeleze na wasipoviendeleza tunawanyang’anya tunawapa watu wengine,” alisema Rais Magufuli.

“Lazima wapate kazi. Haiwezekani wakapata kazi wakati viwanda vilivyopo vingine vimekuwa vya kufugia mbuzi. Wakipewa hivyo viwanda wanakwenda kukopa kwenye mabenki kwamba wanakwenda kuendeleza viwanda. Badala ya kuendeleza viwanda wanakwenda kununua mabasi na vitu vingine,” aliongeza Rais Magufuli huku akishangiliwa muda wote.

 

 

Mawaziri wa Zamani, Mramba na Yona wahukumiwa kufanya usafi Hospitalini, kifungo cha nje
Unataka kumhonga B 12 ili apige wimbo wako redioni? Hiki ndicho atakachokufanyia