Msafara wa Rais Dkt. John Magufuli uliokuwa ukielekea wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, umepata ajali katika Kijiji cha Kasuguti, kata ya Kisorya, leo Septemba 4, 2018 baada ya magari manne kugongana katika eneo ambalo barabara ilikuwa ikijengwa.

Taarifa za awali zinadai kuwa, waandishi wawili wa habari wamejeruhiwa baada ya gari walimokuwa kupinduka.

Amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni vumbi lilikuwa limetapakaa barabarani kutokana na msafara huo hivyo madereva kushindwa kuona vizuri njia lakini hakuna madhara makubwa licha ya gari moja kubondeka ubavuni baada ya kupinduka.

Ameongeza kuwa, magari yote yameshafika eneo la ambalo Rais Magufuli amekwenda kufanya ziara wala hakuna taarifa ya mtu aliyepelekwa hospitali kwa kuumia.

Taarifa nyingine kutoka eneo la tukio zinadai kwamba gari lingine lililopata ajali ni la Chama Cha Mapinduzi mkoa.

Error: Contact form not found.

Error: Contact form not found.

Error: Contact form not found.

 

BREAKING: Rais Magufuli akizungumza na wananchi Ukerewe
Claudio Marchisio afuata nyayo za Spalletti, Mancini