Msako wa waliohusika katika upotevu wa makontena yaliyokwepa kodi bandarini umegeuka kuwa dili mtaani baada ya jeshi la polisi kutangaza kitita cha shilingi milioni 20 kwa watakaofanikisha zoezi la kumnasa mshukiwa.

Kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa jeshi hilo litatoa zawadi ya shilingi milioni 20 kwa mtu yeyote atakayesaidia kukamatwa kwa aliyekuwa wakala wa forodha  ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya Reginal Cargo, Abdulkadil Khasim.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, uchunguzi unaonesha kuwa Khasim ndiye aliyeshughulikia utoaji wa makontena 329 bila kulipiwa kodi na ushuru.

“Yeyote atakayetoa taarifa za kuwezesha kupatikana kwa mtu huyo atapewa zawadi ya shilingi milioni 20,” alisema Kamanda Kova.

Tangazo hilo la Kamanda Kova limeamsha morali wa watu mbalimbali mitaani ambao wanatamani kitita hicho kiwe chao. Duru zinaeleza kuwa baadhi ya vijana waliokuwa wanamfahamu mtuhumiwa huyo wameanza kufanya msako wao wa kimyakimya ili wafanikishe kumiliki kitita hicho.

Toure Kinara Wa Tuzo Ya BBC Afrika Mwaka 2015
Mchezaji Wa Timu Ya Taifa Ya Honduras Auawa