Katika mitandao ya kijamii Ubuyu uliokuwa ukizungumzwa sana ni kuhusu mastaa wawili mmoja kutoka bongo movie na bongo fleva kuwa wameanzisha penzi jingine la kiserengeti Boy (Kuzidiana Umri) Ukiachilia mbali lile Harmonize na Wolper.

Msami kutoka THT pamoja na Kajala Masanja walianza kusababisha wale wasiopitwa na mambo kujiuliza kunani mbona ukaribu kama umeongezeka sana huku wakijumlisha na lile tukio la siku ya kuzawadiwa gari kwa msami akiwa mazoezini Kajala nae kuonekana eneo hilo.

Wawili hao wamezidi kusema wao ni washkaji huku picha za wiwili hao zikisambaa  na kuonesha wana ukaribu zaidi kupitia kipindi cha eNEWS Msami amedai kuwa maneno yanazungumzwa juu yake na Kajala huenda yapo na kama hayapo labda yanaweza kuja kutokea, lakini wao niwashikajiambao wamekuwa wakishirikiana na kusaidia mambo mengi.

“Unajua Kajala ni mtu wangu wa karibu sana, tunaongea mengi na kushauriana vingi japo ukaribu wetu umetafsiriwa tofauti na baadhi ya watu wakidhani tunatoka kimapenzi, japo si vibaya kwani sioni kama kuna ubaya mimi kutoka na Kajala. Sijasema nina mahusiano na Kajala ila ikitokea tukawa wapenzi tunaweza kuzungumza mimi na yeye kujua hatma yake na mume wake ambaye anatumikia kifungo kwa sasa” alisema Msami

Kajala na Quick Racka

kumbukumbu zinaonesha  Msami ni mwanaume wa tatu kuhusishwa kutoka kimapenzi na Kajala siku za karibuni huku Diamond Plutnumz akiwa ametajwa ukiachilia mbali msanii kutoka Mbeya Quick Rocka ambaye yeye mpaka tattoo ya jina la bibie limechorwa kifuani.

Hata hivyo Msami ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa ‘Mabawa’ amesema  kuwa yeye ni mwanaume na Kajala ni mwanamke hivyo kwa kile ambacho kinazungumzwa na watu kuwa huenda anatoka naye kimapenzi si jambo baya kwani Kajala ni mtoto wa kike na yeye ni mwanaume hivyo chochote kinaweza kutokea kati yao.

 

Video: "Tuliahidi kutoa Kero kwa Wananchi..." - Rais Magufuli
Everton Wataja Bei Ya Romelu Lukaku