Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli ameunda tume ya watu 9 ambao watakuwa na jukumu la kufuatilia na kuhakiki mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kote nchini katika wajumbe hao yupo Wakili Albert Msando.

Ameyasema hayo kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kikao chake cha kwanza ambacho kimefanyika mjini Dodoma.

Hata hivyo, Ris Dkt. Magufuli amewataka watu ambao wanashikilia mali za chama hicho wajitokeze na kutoa ushirikiano kwa watu hao huku akiwasisitiza wanachama wa CCM nao kutoa ushirikiano ili mali zao zisipotee.

Video: Waliouza Airtel wakalia kaa la moto, Chadema yajitosa Singida Kaskazini
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 21, 2017